إعدادات العرض
Namna ya kuoga janaba
Namna ya kuoga janaba
Imepokelewa kutoka kwa Maimuna mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilimuandalia kuoga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamfunika nguo, na akamimina maji juu ya mikono yake na akaiosha, kisha akamimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kwa hiyo, akaosha sehemu zake za siri na kuzisafisha, akapiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha, kisha akasukutua kinywa chake na akapandisha maji puani, na akaosha uso na mikono, kisha akamwagia maji kichwani kwake na akaeneza mwili mzima, kisha akasogea pembeni na akaosha miguu yake, nikampa nguo, lakini hakuichukua, akaondoka huku akifuta mikono yake.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල دری অসমীয়া ไทย አማርኛ Svenska Кыргызча Yorùbá ગુજરાતી नेपाली Oromoo മലയാളം Română Nederlands Soomaali پښتو తెలుగు Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Malagasy Српски Moore ქართულიالشرح
Mama wa Waumini Maimuna Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alitueleza jinsi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alivyokuwa akioga janaba, kiasi kwamba alimuwekea maji ya kuoga, na akamfunika kwa pazia, basi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akafanya yafuatayo: Kwanza: Alimimina maji kwenye mikono yake na akaiosha kabla ya kuiingiza katika chombo. Pili: Alimimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto na kuosha sehemu zake za siri ili kuisafisha kutokana na athari yoyote ya janaba. Tatu: Aliipiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha ili kuondoa udhia. Nne: Alisukutukua; Kwa kuingiza maji katika kinywa chake na kuyazungusha, kisha kuyatema; na akavuta maji puani kwa pumzi yake, kisha akayatoa nje ili kuisafisha. Tano: Aliosha uso wake na mikono yake. Sita: Alimimina maji juu ya kichwa chake. Saba: Alimimina maji katika mwili wake mzima. Nane: Alitoka mahali alipoogea na akaosha miguu yake katika mahali pengine, kwani hakuiosha mwanzo. Kisha akamletea kitambaa ili ajifute kwacho, akawa hakukichukua, na akaanza kufuta maji kutoka mwilini kwake kwa mkono wake, na anayapangusa.فوائد الحديث
Wake za Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, walitilia umuhimu wa kutoa sifa nyeti kabisa ya maisha yake; kwa ajili ya kuufundisha umma.
Namna hii ya kuoga ni miongoni mwa namna ambazo zimethibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sifa kamili ya kuoga janaba. Ama namna inayotosheleza ni mtu kueneza mwili wake maji, pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.
Kufuta mwili kwa kitambaa au kuacha baada ya kuoga au kutia udhu ni halali.
التصنيفات
Kuoga.