kuna Aya ndani ya kitabu chenu hua mnaisoma, laiti ingelikuwa imeteremka kwetu sisi jamii ya Mayahudi, basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu

kuna Aya ndani ya kitabu chenu hua mnaisoma, laiti ingelikuwa imeteremka kwetu sisi jamii ya Mayahudi, basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu

Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: Kuwa mwanume mmoja katika Mayahudi alisema kumwambia: Ewe kiongozi wa waumini, kuna Aya ndani ya kitabu chenu hua mnaisoma, laiti ingelikuwa imeteremka kwetu sisi jamii ya Mayahudi, basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu, akasmea: Ni Aya ipi? Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." [Al-Maaida: 3] Omari akasema: Tunaijua siku hiyo, na mahali ilipoteremka aya hiyo kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa kasimama Arafa siku ya Ijumaa.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alikuja mtu mmoja katika Mayahudi kwa kiongozi wa waumini Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Kuna aya ndani ya kitabu chenu cha Qur'ani mnaisoma, lau ingeliteremka kwetu jamii ya Mayahudi katika kitabu chetu cha Taurati basi tungeifanya siku hiyo kuwa sikukuu kwa kuisherehekea; kwa kushukuru neema ya kuteremka aya hii tukufu, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema kumwambia: Ni Aya ipi?. Akasema: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." Akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Tunaijua siku hiyo, na sehemu iliyoteremka aya hii tukufu, aya hiyo imeteremka siku ya Iddi, nayo ni siku ya Ijumaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa amesimama Arafa, nazo ni siku mbili tukufu kwa Waislamu.

فوائد الحديث

Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kutilia umuhimu mahali zilipoteremka aya na wakati wake.

Aya hii kuna uwazi juu ya yale aliyouneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Umma huu, kiasi kwamba aliikamilisha dini, na akaitimiza neema yake juu yake, kiasi kwamba haihitaji ziada katika jambo la dini, yote yaliyozuka baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuikamilisha dini, katika yale yasiyokuwa na ushahidi kutoka kwake, yanazingatiwa kama uzushi na upotofu, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayezua katika dini yetu hii, yale yasiyokuwemo, basi yatarejeshwa".

Hadithi hii inaweza kuchukuliwa kuwa sikukuu haziwi kwa mtazamo na ubunifu kama wafanyavyo watu wa vitabu viwili kabla yetu; bali zinakuwa kwa sheria na kufuata mafundisho, aya hii baada ya kufungamana na kukamilika kwa dini na kutimia kwa neema aliiteremsha Mwenyezi Mungu katika siku ya kuweka kwake sheria ya sikukuu kwa Umma kwa namna mbili: Ya kwanza: Nikuwa hiyo ni sikukuu ya wiki ambayo ni siku ya Ijumaa. Na ya pili: Ni kuwa ni sikukuu ya watu wa msimu, ambayo ndiyo siku ya mkusanyiko wao mkubwa, na kisomamo chao kikubwa.

Amesema Assaady katika kutafsiri aya hii: "Leo nimekukamilishieni dini yenu" kwa kutimia kwa kushindo, na kukita mizizi sheria ya wazi na ya siri, sehemu zake na misingi yake, na ndio maana Qur'ani na Sunna vimetosheleza kila kitu kabisa, katika hukumu za dini, misingi yake na matawi yake, kila mwenye kujilazimisha anayedai kuwa ni lazima watu wajue itikadi zao na hukumu zao kupitia elimu zisizokuwa Qur'ani na Sunna, kama elimu ya Falsafa, huyu ni mjinga, na ni mtu batili katika madai yake, na atakuwa amedai kuwa dini haikamiliki isipokuwa kwa yale aliyoyasema na kuwaita watu kwayo, na hii ni miongoni mwa dhuluma kubwa na ni kumfanya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa hawajui lolote, "na nimekutimizieni neema zangu" za wazi na za siri, "na nimeridhia kwenu Uislamu kuwa ndio dini" yaani: nimeichagua na kuiteua kuwa ndio dini kwenu, kama nilivyokuridhieni kwa dini hiyo, basi isimamieni kama shukurani kwenu, na mshukuruni yule aliyekuneemesheni kwa dini bora kuliko zote, na tukufu na kamilifu zaidi.

التصنيفات

Fadhila za Sura na Aya.