إعدادات العرض
Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?
Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?
Kutoka kwa Abuu Dardai -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".
الترجمة
العربية Português دری Македонски Magyar Tiếng Việt ქართული Kurdî বাংলা ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Bahasa Indonesiaالشرح
Aliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.فوائد الحديث
Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuwauliza Maswahaba zake na kuwatia shauku ya kujua jawabu.
Amesema Al-Twayyibi: Himizo na hamasa ya kusuluhisha baina ya watu na kujiepusha na kuwavuruga; kwa sababu kutengemaa ndio sababu ya kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kutofarakana baina ya Waislamu, na kuharibu mahusiano ni pengo katika dini, na atakeyejitosa kulirekebisha na kuondoa uharibifu wake atapata daraja la juu zaidi ya lile analolipata mfungaji mwenye kusimama usiku mwenye kujishughulisha na nafsi yake pekee.
