إعدادات العرض
Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi
Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi
Kutoka kwa Abdallah bin Nu'man bin Bashiri -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Yorùbá Lietuvių دری Српски Soomaali тоҷикӣ Kinyarwanda Română Magyar Čeština Moore Malagasy Fulfulde Italiano Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Български Azərbaycan Ελληνικά Akan O‘zbek Українська ქართული Lingala Македонски ភាសាខ្មែរ Bambara ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayu Yaoالشرح
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake. Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.فوائد الحديث
Hadithi hii ni kanuni katika kuepuka mambo yenye utata.
Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.
