إعدادات العرض
Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia
Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia". Akasema: Akasema Al-Ash'athi: Kwangu mimi Wallahi kulitokea tukio hilo; kulikuwa na Ardhi baina yangu na bwana mmoja Yahudi, akanipinga kuwa si yangu, nikampeleka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuniambia: "Je una ushahidi?" Nikasema: Hapana: Akasema kumwambia Yahudi: "Toa kiapo". Anasema: Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sasa si ataapa na atachukua mali yangu!. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo..." mpaka mwisho wa aya.
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Türkçe اردو 中文 हिन्दी Português മലയാളം Kurdî Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu huku muapaji akijua kuwa anaapia uongo ndani yake, ili ajipatie kwa kiapo hiki mali ya mwenzake; huyu atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia, akaeleza Ash'athi bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilisema hilo wakati ambao kulikuwa na mzozo kati yake yeye na bwana mmoja Yahudi katika umiliki wa Ardhi, wakashitakiana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia Ash'athi: Unatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha madai yako, ukishindwa kuuleta basi hutokuwa na haki zaidi ya kiapo cha hasimu wako mshitakiwa, Ash'athi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi huyu bwana Yahudi si ataapa pasina hofu na mali yangu itapotea, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kusadikisha hilo ndani ya Qur'ani kauli yake Mtukufu: "Hakika wale wanaouza" na wanabadilisha "ahadi ya Mwenyezi Mungu", na usia wake kwa waumini kwa kutimiza amana "na viapo vyao" na viapo vyao kwa jina lake kwa uongo "kwa thamani ndogo" kwa starehe za dunia "Hao hawana fungu lolote kwao Akhera" wala sehemu "Wala hatowasemesha Mwenyezi Mungu", kwa maneno yanayowafurahisha na kuwanufaisha, bali atawaghadhibikia, "wala hatowatazama siku ya Kiyama", mtazamo wa huruma na wema, "wala hatowatakasa" kwa kuwasifia kwa mazuri, wala hatowasafisha kwa kuwapa msamaha wa madhambi na machafu "na watakuwa na adhabu chungu" yenye kuumiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya.فوائد الحديث
Uharamu wa kuhalalisha mali za watu kwa dhulma.
Uzito wa haki za waislamu katika kidogo na kingi.
Ushahidi kwa mwenye kudai, na kiapo kwa mlalamikiwa atakapokataa.
Haki inathibiti kwa mashahidi wawili, usipopatikana ushahidi kwa mlalamikaji, basi ni lazima kwa mlalamikiwa kutoa kiapo.
Uharamu wa kiapo cha (kuzama) nacho ni kiapo cha uongo ambacho muapaji anajikatia haki ya mtu mwingine, nalo ni katika madhambi makubwa, ambalo linamtia mtu katika ghadhabu za Mwenyezi Mungu Mtukufu na adhabu zake.
Nasaha za hakimu wakati wa mzozo, hasa hasa wakati wa kutaka kiapo.