Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa

Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa

Kutoka kwa Ummu Dardaai na Abuu Dardaai radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa, kichwani kwake huwa kuna Malaika aliyepewa kazi, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, Malaika aliyepewa kazi hiyo husema: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua, na kwako pia upate mfano wake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua ya muislamu kwa ndugu yake muislamu, anapokuwa hayupo anayeombewa dua, hujibiwa; kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha utakasifu (Ikhlaswi) na kwamba kichwani kwa muombaji huwa kuna Malaika aliwakilishwa, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, basi anasema Malaika alipewa kazi hiyo: Mwenyezi Mungu apokee dua, na upate pia mfano wa hayo uliyoomba.

فوائد الحديث

Himizo kwa waumini la kutendeana wema wao kwa wao walau hata kwa dua.

Dua ya siri inaonyesha dalili wazi juu ya imani ya kweli na udugu.

Kufungamanishwa dua na siri; ni kwa sababu hilo huwa katika kiwango kikubwa cha utakasifu, na kuhudhuria moyo.

Miongoni mwa sababu za kujibiwa dua ni mtu kumuombea ndugu yake kwa siri.

Amesema Nawawi: Fadhila ya dua kwa ndugu yake muislamu kwa siri, na hata akiwaombea watu wengi katika waislamu pia atapata fadhili hii, na hata akiwaombea waislamu wote kwa ujumla, pia inavyoonekana atapata fadhila hizi, na walikuwa baadhi ya wema waliotangulia anapotaka kujiombea mwenyewe basi anamuombea ndugu yake muislamu dua hiyo; kwa sababu inajibiwa, na yeye anapata mfano wake.

Hapa kumebainishwa baadhi ya kazi za Malaika, na kwamba wako miongoni mwao aliowapa Mwenyezi Mungu kazi hii.

التصنيفات

Kuamini Malaika, Fadhila za Dua.