Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu.

Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu.

Kutoka kwa Adiy bin Hatim-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Akisoma aya hii: "Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, na hawakuamrishwa ila ni kumuabudu Mungu mmoja, hapana Mola ispokuwa yeye, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" Nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao, Akasema: "Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Aliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.

فوائد الحديث

Nikuwa kuwatii wanachuoni na wengineo katika viumbe katika kubadili hukumu za Mwenyezi Mungu-ikiwa mwenye kuwatii anajua kuwa huko ni kwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu- ni shirki kubwa.

Nikuwa kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kubainishwa kwa aina miongoni mwa aina za shirki, nayo ni shirki ya kutii.

Sheria ya kumfundisha mjinga.

Nikuwa maana ya ibada ni pana, inakusanya yote anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika maneno na matendo ya wazi na ya siri.

Kubainishwa upotofu wa wanachuoni na watawa.

Kuthibitishwa kwa ushirikina wa Mayahudi na Wakristo.

Nikuwa, asili ya dini ya Mitume ni moja, nayo ni Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu).

Nikuwa kumtii kiumbe katika kumuasi muumba nikumuabudu.

Ulazima wa kutaka ufafanuzi kutoka kwa wenye elimu kwa yale ambayo hukumu yake imefichikana.

Pupa ya maswahaba juu ya elimu.

التصنيفات

Ushirikina.