Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu

Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu, na toeni bishara, na takeni msaada nyakati za asubuhi au mchana au sehemu ya usiku"

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Alibainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Dini ya Uislamu imeegemezwa katika usahilishaji na wepesi katika mambo yake yote, na usahilishaji unathibitishwa pale panapotokea sababu ya kutokuwa na uwezo na haja, kwa sababu kuzama ndani sana katika matendo ya dini na kuacha upole matokeo yake ni kutoweza na kukoma kufanya amali zote au baadhi yake. ... Kisha akahimiza rehema na amani ziwe juu yake kuwa kati na kati pasina kupitiliza; Mja asifanye uzembe katika yale aliyoamrishwa, na wala asijibebeshe asiyoyaweza, akishindwa kuifanya amali nzima kamili; basi afanye inayokaribiana na hiyo. Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya malipo makubwa ya amali ya kudumu, hata ikiwa ni kidogo, kwa wale ambao hawawezi kufanya amali nzima kikamilifu, kwa sababu ikiwa kushindwa huko hakutokani na yeye mwenyewe, hakutopelekea kupunguzwa kwa malipo yake. Na kwa kuwa ulimwengu huu kwa hakika ni mahala pa kusafiri na mapito ya kuelekea Akhera, ameamrisha rehema na amani ziwe juu yake kutaka msaada katika kudumisha ibada kwa kuiweka nyakati tatu ambazo mtu anakuwa na hamasa: Wakati wa kwanza ni Asubuhi: Kwa kwenda mwanzo wa mchana; kati ya swala ya Alfajiri na kuchomoza jua. Wa pili: Mchana: Kwa kwenda wakati linapopinduka jua. Wa tatu: Giza: kwa mwendo wa usiku mzima au sehemu yake, na kwa sababu amali ya usiku ni ngumu zaidi kuliko amali ya mchana, akaamrisha kufanya baadhi yake, kwa kauli yake: Na baadhi ya usiku.

فوائد الحديث

Wepesi na urahisi wa sheria ya Uislamu, na kuwa kwake ya kati na kati, kati ya uzembe na mkazo.

Mja analazimika kufanya matendo kwa kadiri ya uwezo wake, pasina kupuuza au kutia mkazo.

Ni lazima mja achague nyakati za kuwa na uchangamfu katika ibada, na nyakati hizi tatu ndizo nyakati bora ambazo mwili unakuwa na uchangamfu katika ibada.

Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Ni kana kwamba rehema na amani ziwe juu yake amemuelekeza msafiri mahali pa kupelekwa, na nyakati hizi tatu ndizo nyakati bora kwa msafiri, hivyo akamzindua nyakati za uchangamfu wake; Kwa sababu ikiwa msafiri atasafiri mchana na usiku mzima, atakuwa hana uwezo na akakatikiwa, na ikiwa atajitahidi kutembea katika nyakati hizi za uchangamfu basi ataweza kudumu bila tabu.

Amesema bin Hajar: Hadithi hii inaashiria kuchukua ruhusa ya kisharia, kwa sababu kufanya ulazima mahali pa ruhusa ni ukiukaji, sawa na mtu anayeacha tayammam wakati hana uwezo wa kutumia maji na kuyatumia kwake kukapelekea kuleta madhara.

Amesema bin Munir: Hadithi hii ni miongoni mwa alama za unabii, kwa hakika tuliona na watu waliotangulia pia waliona kuwa kila mwenye kupita kiasi katika dini huishia njiani, na makusudio yake si kuzuia kutaka ukamilifu katika ibada, kwani ni katika mambo ya kusifiwa, bali ni kuzuia uzembe unaopelekea katika uvivu, au kupita mipaka katika jambo la sunna kunakopelekea kuacha kilicho bora, au kuitoa faradhi nje ya wakati wake, kama vile mtu aliyekesha usiku kucha kisha akalala na akapitwa na Swala ya Alfajiri kwa jamaa, au mpaka jua likachomoza na muda wa kuswali ukatoka.

التصنيفات

Ubora wa uislamu na uzuri wake.