Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu…

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa

Kutoka kwa Zaidi bin Arqam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sikwambieni isipokuwa kama alivyokuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako" na ninajiegemeza kwako, "Kutokana na kushindwa" kwa kukosa uwezo wa unjanja wenye manufaa, "na uvivu" kwa kushindwa kuendesha mambo, aliyeshindwa hana ujanja, na mvivu hana haja nao, "na uoga" kwa kujizuia kuyaendea yanayopasa kufanywa, "na ubahili" kwa kuzuia yanayopaswa kuyatoa, "na ukongwe" na ukubwa wa umri unaopelekea udhaifu wa mwili, "na adhabu za kaburi" na sababu zinazopelekea katika hayo. "Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu" na uipe na uiwezeshe katika "uchamungu wake" kwa kufanya uchamungu na kuacha maasi, "na uitakase" na uisafishe kutokana na uchafu na tabia mbaya, "wewe ndiye mbora wa kuitakasa" na wala hakuna wa kuitakasa yeyote zaidi yako, "Wewe ndiye msimamizi wake" na mtetezi wake na msimamizi wake, "na Mola wake" Msimamizi wa mambo yake, na Mola wake Mlezi na mwenye kuineemesha. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa", kama elimu ya nyota na ukuhani na uchawi, au isiyo na manufaa Akhera, au elimu isiyofanyiwa kazi, "na moyo usionyenyekea" kwako, na wala haujishushi, na wala hautulii, wala hautulizani kwa kukutaja, "na nafsi isiyoshiba" wala isiyokinai kwa yale iliyopewa na Mwenyezi Mungu na akairuzuku miongoni mwa halali nzuri, "na kutokana na maombi" yenye kurudishwa "yasiyopokelewa".

فوائد الحديث

Ni sunna kuomba kinga dhidi ya mambo haya yaliyotajwa katika hadithi.

Himizo juu ya uchamungu na kusambaza elimu na kuifanyia kazi.

Elimu yenye manufaa inayoitakasa nafsi na kuizalishia hofu ya Mola Mlezi Aliyetakasika na kutukuka, na kutiririka katika viungo vingine vilivyobakia.

Moyo wenye unyenyekevu ni ule unaoogopa na kutaharuki wakati wa kutajwa Mwenyezi Mungu kisha ukalainika na kutulia.

Chukizo la kuipupia dunia na kutoshiba kutokana na matamanio yake na ladha zake, na ndio maana nafsi inayotokota yenye pupa na starehe za dunia ndio adui mkubwa wa mtu, na ndio maana alijikinga dhidi yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Inampasa mja ajitenge mbali na sababu za kukataliwa dua na kutojibiwa kwake.

Amesema Nawawi: Hadithi hii na nyinginezo ni miongoni mwa dua zenye vina, ni ushahidi waliousema wanachuoni; kuwa vina visivyotakiwa katika dua ni vile vya kujikalifisha, kwani huondoa utulivu na unyenyekevu na utakasifu, na hupumbaza na kuacha kujinyenyekeza na moyo kuwa mtupu, ama inayofanyika bila kujikalifisha wala kushughulisha akili kwa sababu ya ukamilifu wa ufasaha na mfano wake, au ikawa mtu kaihifadhi, hii haina ubaya, bali ndio nzuri.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.