إعدادات العرض
Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe
Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba mtu mmoja aliyeandikishana kujitoa katika utumwa alimjia akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni tuliloandikishana, basi naomba unisaidie, akasema: Je, nikufundishe maneno ambayo alinifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hata kungekuwa juu yako na deni zito mfano wa mlima Swiri Mwenyezi Mungu atakulipia, akasema: "Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français ئۇيغۇرچە Kurdî Русский Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Alimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.فوائد الحديث
Kuomba ushauri na kutaka rai ya wasomi wa dini.
Ni juu ya wasomi na walimu wa dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa muongozo walinganiaji, na kuwaelekeza katika yale yanayoweza kuwasaidia kwa yale yanayowatokea miongoni mwa matatizo.
Himizo la kumsaidia mwenye mkataba.
Himizo la kujifunza dua hii, na kumuomba Allah kupitia dua hii.
Riziki ya halali hata ikiwa ndogo, ni bora kuliko mali ya haramu hata ikiwa nyingi.
Kutosheka na Mwenyezi Mungu na kuwaacha viumbe.
Himizo la kumjibu muombaji kwa majibu mazuri ikiwa huna cha kumpa.
التصنيفات
Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.