Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha

Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuitundika dua na chochote hata ikiwa kwa matashi ya Mwenyezi Mungu; kwa sababu hilo ni jambo linalojulikana na ni la uhakika kuwa hasamehi mpaka atake Mtukufu, na haina maana kuweka sharti la matashi; kwa sababu huwekwa sharti hilo kwa yule ambaye anaweza kufanya pasina kutaka kwa kulazimishwa na vinginevyo ambavyo Mwenyezi Mungu ametakasika navyo Mtukufu, na amelibainisha hilo rehema na amani ziwe juu yake mwisho wa hadithi kwa kauli yake kuwa hakuna wa kumlazimisha, kama Mwenyezi Mungu hakuna kinachokuzwa kwake ila anakitoa na wala hakuna kinachomshinda au kikawa kikubwa kwake chochote mpaka tuseme: Ukitaka, na kuutundika msamaha na matashi ni aina ya kutokuuhitaji msamaha wake, kauli ya mtu kusema: Ukitaka kunipa kadhaa basi nipe, huwa haitumiki kauli hiyo ila pale mtu anapokuwa hana haja au kwa asiyeweza, ama kwa anayeweza na pamoja na uhitaji wake basi anatakiwa kudhamiria kuomba, na aombe maombi ya masikini aliyedhikika mwenye uhitaji, na ajiweke karibu na Mwenyezi Mungu; kwa sababu yeye ndiye tajiri kamili, muweza juu ya kila kitu.

فوائد الحديث

Katazo la kutundika dua na matashi.

Kumtakasa Mwenyezi Mungu na yale asiyostahiki, na upana wa fadhila zake, na ukamilifu wa utajiri wake, na ukarimu wake na ukwasi wake Aliyetakasika na kutukuka.

Kuthibitisha ukamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kukuza shauku kwa yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu na dhana nzuri kwake Mtukufu.

Baadhi ya watu huingia katika kuitundika dua pasina wao kujua, mfano kama kauli: Allah akulipe kheri In shaa Allah, Allah amrehemu In shaa Allah, hii haifai kwa mujibu wa hadithi ya mlango huu.

التصنيفات

Adabu za Dua.