إعدادات العرض
1- Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi
2- Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu
3- Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu
4- Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo
5- Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha