Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo.

[Sahihi]

الشرح

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua zenye kukusanya kheri za dunia na Akhera ambazo matamshi yake ni machache na maana yake ni nyingi, na kunakuwa ndani yake na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na malengo mazuri, na anaachana na yasiyokuwa hayo.

فوائد الحديث

Kupendeza kuomba dua kwa matamshi machache yenye kukusanya maana nyingi za kheri, na karaha ya kujikalifisha na kujitia tabu katika kuomba, jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipendelewa kwa kuwa na maneno machache yenye kukusanya maana pana.

Kupupia yaliyothibiti kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kwa maombi hayo; hata kama dua ikiwa ndefu, na maneno yake yakawa mengi, yote ni katika dua zilizokusanya maana pana.

التصنيفات

Adabu za Dua.