إعدادات العرض
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu
Na kutoka kwa Salmani -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu".
[Ni nzuri]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Português தமிழ் অসমীয়া ગુજરાતીالشرح
Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kunyanyua mikono wakati wa dua, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "huona haya" mwingi wa haya, na haachi kutoa, anamfanyia mja yenye kumfurahisha, na anaacha yenye kumdhuru, "Ni Mkarim" hutoa pasina kuombwa, je hali huwaje baada ya kuombwa! anamuonea haya mja wake muumini kuirejesha patupu mikono yake baada ya kuinyanyua kwa ajili ya dua ikiwa imefeli haina kitu kwa kutojibiwa.فوائد الحديث
Kila anapodhihirisha mwanadamu unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumuabudu, ndivyo inavyotarajiwa kwake kuwa na ukaribu wa kujibiwa.
Himizo la kuomba dua, na kupendeza kunyanyua mikono ndani yake, nakuwa kufanya hivyo ni katika sababu za kujibiwa.
Kumebainishwa upana wa ukarimu wa Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa waja wake .
التصنيفات
Adabu za Dua.