Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake

Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الترجمة

ar bn bs en es fa fr id ru tl tr ur zh hi vi si ku nl as gu hu ka ha ro

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba siku moja kuna mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akapita katika tawi mti wa miba likiwa barabarani likiwaudhi waislamu, akalivuta na akaliondosha njiani, basi Mwenyezi Mungu akamshukuru na akamsamehe.

فوائد الحديث

Fadhila za kuondoa udhia njiani, na kwamba hilo ni sababu ya kuupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.

Kutodharau matendo mema hata yakiwa ni madogo.

Uislamu ni dini ya usafi na kulinda mazingira na amani ya jamii nzima.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.