إعدادات العرض
Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili
Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili
Kutoka kwa Abdallah bin Zubairi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
الترجمة
ar en my sv cs gu yo nl ur id ug bn tr si hi vi ha te ps as prs ky lt rw ne ml bs kn ku ro so sq sr uk wo mos tl ta az fa ka zh hu pt de ru mk bm am mg omالشرح
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara mbili, anaosha uso ikiwemo kusukutua na kupandisha maji puani na mikono miwili na miguu miwili mara mbili.فوائد الحديث
Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja na kinachozidi inapendeza.
Sheria ya kutia udhu mara mbili mbili katika baadhi ya nyakati.
Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.