إعدادات العرض
1- Yeyote atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili, na asiizungumzishe ndani ya nafsi yake atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
2- Nilimshuhudia Amru bin Abii Hasan alimuuliza Abdullah bin Zaidi kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha kwaajili yao udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake
3- Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja
4- Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili