Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu

Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu

Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".

الشرح

Alisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kutia udhu kwa ajili ya swala ya Alaasiri baadhi ya Masahaba, mpaka ukaonekana weupe mwisho wa miguu yao kwa mtu mwenye kuitazama kwa kukosa maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni adhabu na maangamivu katika moto kwa wenye kufanya uzembe wa kuosha mwisho wa nyayo wakati wa udhu, na akawaamrisha wapitilize katika kuukamilisha udhu.

فوائد الحديث

Ulazima wa kuosha miguu miwili katika udhu; kwa sababu lau kama ingefaa kufuta asingetoa ahadi ya adhabu ya moto kwa mwenye kuacha kuosha mwisho wa miguu yake.

Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vyenye kuoshwa wakati wa udhu, nakuwa atakayeacha sehemu ndogo ambayo ni ya wajibu kusafishwa kwa makusudi au kwa uzembe, basi swala yake haisihi.

Umuhimu wa kumfundisha asiyejuwa na kumuelekeza.

Msomi anatakiwa kukemea anayoyaona ikiwemo kupoteza wajibu na sunna, lakini kwa usulubu mzuri.

Amesema Muhammad Is-haqa Al-Dahalawi: Kueneza maji kuna aina tatu: Lazima (Faradhi) Nako ni kueneza maji mahali unapoosha kwa mara moja, na sunna: Nayo nikuosha kiungo mara tatu, na inapendeza:

kurefusha mahali unapoosha ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo mara tatu.

التصنيفات

Sifa za Kutawadha.