Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia

Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia

Imepokelewa kutoka kwa Humran kijana wa Othman bin Affan alimuona Othman bin Affan akiomba kuletewa chombo cha udhu, akamimina juu ya mikono yake kutoka katika chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia katika chombo, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga(akayatoa), kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara tatu, kisha akafuta kichwa chake, kisha akaosha kila mguu mara tatu, kisha akasema: Nilimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu wangu huu, na akasema: "Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- alifundisha sifa ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa njia ya vitendo; Ili ueleweka vizuri zaidi, akaomba maji katika chombo, akamimina katika mikono yake mara tatu, na baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo, na akachukua maji akayazungusha kinywani mwake na akayatoa, kisha akavuta kwa pumzi yake kuja ndani ya pua yake, kisha akayatoa na akayapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko viwili mara tatu, kisha akapitisha mkono wake juu ya kichwa chake ukiwa umeloa kwa maji mara moja, kisha akaosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu. Alipomaliza radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu huu, na akawapa bishara -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa utulivu na kuhudhuriasha moyo mbele ya Mola wake Mtukufu ndani yake, basi Allah atamlipa kwa udhu huu mkamilifu na kwa swala hii iliyotakaswa kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.

فوائد الحديث

Inapendeza kuosha mikono miwili kabla ya kuiingiza katika chombo mwanzo wa udhu, hata kama hajaamka kutoka usingizini, na akiwa kaamka kutoka usingizini basi ni wajibu kuiosha.

Ni lazima mwalimu atumie njia ya karibu na uelewa na kuifanya elimu ikite kwa mwenye kujifunza, na katika hilo ni kufundisha kwa vitendo.

Ni lazima kwa mwenye kuswali kuzuia mawazo yanayohusiana na shughuli za kidunia, utimilifu wa swala na ukamilifu wake ni katika kuhudhuria moyo ndani yake, na kama si hivyo mawazo ni vigumu kusalimika nayo, anatakiwa apambane na nafsi yake na asiruhusu yaendelee.

Sunna ya kuanza na kulia katika udhu.

Sheria ya kupangilia kati ya kusukutua na kupandisha maji puani na kupenga.

Sunna ya kuosha uso na mikono miwili na miguu miwili mara tatu tatu, na wajibu ni mara moja.

Mwenyezi Mungu kuyasamehe yaliyotangulia katika madhambi kunaambatana na mambo mawili: Udhu, na kuswali rakaa mbili, kwa sifa iliyotajwa katika hadithi.

Kila kiungo katika viungo vya udhu kina mpaka: Mpaka wa uso: Kwa urefu ni kuanzia maoteo ya nywele za kichwa ya kawaida, mpaka chini katika ndevu na kidevu, na kwa upana ni sikio kwa sikio. Na mpaka wa mkono: Ni kuanzia ncha za vidole mpaka katika kiwiko nayo ni maungio kati ya muhundi na sehemu ya juu kuelekea begani. Na mpaka wa kichwa: Ni kuanzia maoteo ya kichwa ya kawaida kando kando ya uso mpaka juu ya shingo, na kufuta masikio mawili ni sehemu ya kichwa. Na mpaka wa mguu ni: Mguu wote pamoja na maungio kati yake na muhundi.

التصنيفات

Sifa za Kutawadha., Sifa za Kutawadha.