Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba

Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake msimamizi wa mwanamke na muhusika wake kuwakataza wanawake kwenda Msikitini, na akawaamrisha wanawake wakati wa kutoka kwenda Msikitini watoke bila kujipuliza manukato na wasitoke kwa kujiachia kwa mapambo; ili wasiwe sababu ya fitina kwa wanaume.

فوائد الحديث

Kumpa ruhusa mwanamke ya kwenda kuswali Msikitini atapokuwa na uhakika wa kutopata fitina, na akatoka bila mapambo wala manukato.

Wameitumia hadithi hii kama ushahidi kuwa mwanamke hatoki nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake, kwakuwa amri ya idhini imeelekezwa kwa wanaume.

Uislamu umewapa kipaumbele wanawake, na kutowazuia kwa mambo ambayo yanaweza kuwa ni heri kwao kama kutoka kwenda kutafute elimu na mfano wake.

Kuthibiti kwa usimamizi wa mwanaume juu ya mwanamke na kumchunga.

التصنيفات

Mavazi na Mapambo., Hukumu za Misikiti.