Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura

Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura, na walau wangelijua yaliyomo katika kuwahi basi wangelishindana, na lau wangelijua yaliyomo katika swala ya usiku na swala ya Asubuhi, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba laiti watu wangelijua yaliyomo katika Adhana na safu ya kwanza miongoni mwa fadhila na kheri na baraka, kisha wakakosa namna ya kutangulizana na nani awe bora kuliko mwingine ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura, na lau wangelijua yaliyomo katika kuwahi swala mwanzo wa wakati wake basi wangelishindana kuyaendea, na laiti wangelijua kiwango cha thawabu katika kuiendea swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, basi kungekuwa kwepesi kuziendea hata kwa kutambaa kwa magoti kama anavyotembea mtoto mwanzo wa kukua kwake.

فوائد الحديث

Kumebainishwa fadhila ya Adhana.

Kumebainishwa fadhila ya safu ya kwanza, na kuwa karibu na imamu.

Kumebanisha ubora wa kuwahi katika swala mwanzo wa wakati wake unaofaa; kwakuwa ndani yake kuna fadhila kubwa, na faida zinazoambatana na hilo, ikiwemo: Kuipata safu ya kwanza, na kuipata swala kuanzia mwanzo wake, na kutekeleza swala za sunna, na kusoma Qur'ani, na kupata kuombewa msamaha na Malaika, na kwamba anapata malipo kana kwamba yupo ndani ya swala kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na mengineyo.

Himizo kubwa la kuhudhuria jamaa za swala hizi mbili, na fadhila nyingi katika hilo, kwa kuwa ndani yake kuna ugumu juu ya nafsi kama kuibana mwanzo wa usingizi wake na mwisho wake, na ndiyo maana zikawa ndio swala ngumu zaidi kwa wanafiki.

Amesema Nawawi: Hapa kuna kuthibitishwa kupiga kura katika haki ambazo watu wanasongamana na kuzozana ndani yake.

Safu ya pili ni bora kuliko safu ya tatu, na ya tatu ni bora kuliko ya nne, na kuendelea.

التصنيفات

Mambo yaliyo bora., Nguzo za Swala.