Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake

Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake, na wala hatokunywa katika Hodhi langu, na ambaye hatowaamini kwa uongo wao na akawa hakuwasaidia katika dhulma yao, basi huyo yuko miongoni mwangu, na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba watatawala watu baada ya kifo chake viongozi wanaosema uongo katika mazungumzo yao wanasema wasiyoyatenda, na wanadhulumu katika hukumu, atakayeingia kwao na akawasadikisha kwa uongo wao, au akawasaidia kufanya dhulma au kuitamka, kama kutoa majibu kwa lengo la kujipendekeza kwao na kutaraji mazuri waliyonayo; basi mimi niko mbali naye na yeye si miongoni mwangu, wala hatokuja katika Hodhi la mto Kauthari siku ya Kiyama, na ambaye hatoingia kwao na kuwasadikisha kwa uongo wao na kuwasaidia juu ya dhulma yao basi huyo ni miongoni mwangu na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu siku ya Kiyama.

فوائد الحديث

Watawala watu wakiingia kwao kwa lengo la kuwaelekeza na kuwapa nasaha na kupunguza shari; jambo hili ndilo linalotakiwa, ama wakiingia kwao kwa lengo la kuwasaidia katika dhulma na kuwasadikisha katika uongo hili ndilo jambo baya.

Kumebainishwa ahadi ya adhabu kali kwa atakayemsaidia kiongozi katika dhulma yake.

Ahadi hii katika hadithi inaonyesha uharamu wa kitendo hiki, na kuwa ni katika madhambi makubwa.

Himizo la kusaidizana katika wema na uchamungu, na kutosaidizana katika madhambi na uadui.

Kumethibitishwa Hodhi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba Umma wake utakunywa hapo.

التصنيفات

7- Adabu za kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya:, Haki ya kiongozi kwa Raia.