Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Hadithil Kudsi: Ananiudhi na ananishusha hadhi mwanadamu anayetukana na kusema vibaya wakati wa kufikwa na matatizo na machukizo; kwa sababu yeye Mtukufu ndiye mpangiliaji peke yake na muendeshaji wa yote yanayotokea; kutukana nyakati ni kumtukana Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na nyakati ni kiumbe na kinaendeshwa, yanatokea matukio ndani yake kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

فوائد الحديث

Hadithi hii ni katika yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithi ya kiuungu, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake imetoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina mambo maalumu kama ya Qur'ani ambayo inatofautiana kwayo na maneno mengine, ikiwemo kukitumia kisomo chake kama ibada na kuwa twahara (msafi) na kutoa changamoto na maswala kisayansi na mengineyo.

Kuwa na adabu na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli na itikadi.

Uwajibu wa kuamini maamuzi na mipango ya Mwenyezi Mungu, na kuwa na subira juu ya maudhi.

Maudhi si madhara; mwanadamu huudhika anaposikia mabaya au kuyaona; lakini hadhuriki kwa hilo, lakini pia anaudhika kwa harufu mbaya kama vitunguu maji na vitunguu thaumu na wala hadhuriki kwa hivyo.

Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka anaudhika kwa baadhi ya matendo mabaya ya waja wake, lakini yeye Aliyetakasika na kutukuka hadhuriki kwa hilo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika hadithil Kudsi: "Enyi waja wangu hakika nyinyi hamtofikia kunidhuru mkanidhuru, na wala hamtofikia kuninufaisha mkaninufaisha".

Kutukana zama na kuisifu kuna gawanyika katika sehemu tatu: 1- Ni atukane zama kuwa yenyewe ndiyo inayofanya hayo; na kwamba zama ndiyo zinazogeuza mambo kwenda katika kheri na shari! Hii ni shirki kubwa; kwa sababu hapa atakuwa kaitakidi kuwa kunamuumba mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, na ni kwa sababu ameambatanisha kupatikana kwa matukio na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, 2- Ni atukane zama si kwa kuitakidi kwake kwamba zama ndio zinazotenda; bali anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtendaji lakini anaitukana kwa sababu ndio mahali pa maudhi haya kwake; hili ni haramu, 3- Akusudie kutoa habari bila kulaumu; hili linafaa, na katika hilo ni pamoja na kauli ya Lutu amani iwe juu yake: "Na akasema hii ni siku ngumu".

التصنيفات

Adabu ya mazungumzo na kunyamaza.