إعدادات العرض
Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni
Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".
[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو हिन्दी Tagalog 中文 ئۇيغۇرچە Kurdî Português Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mja anapokufa huonyeshwa mbele yake makao yake na sehemu yake maalumu peponi au motoni, mwanzo wa mchana na mwisho wake; mahali pake peponi, na sehemu yake motoni akiwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na huambiwa: Haya ndiyo makao yako utakayofufuliwa kwayo siku ya Kiyama; na katika hilo kuna kuneemeka kwa muumini, na kuadhibiwa kwa kafiri.فوائد الحديث
Adhabu za kaburi na neema zake ni kweli.
Amesema bin Hajari: Hakika kuonyeshwa huku kwa muumini na kafiri kuko wazi, na ama muumini aliyechanganya mema na maovu inategemea anaweza kuonyeshwa makao yake katika pepo atakayofikia.
التصنيفات
Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa)