Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba

Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba

Kutoka kwa Baraa bin Azib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba: Alituamrisha kumtembelea mgonjwa, na kusindikiza jeneza, na kumuombea mwenye kupiga chafya, na kukiepusha kiapo au kumuepusha (na tuhuma) aliyeapa, na kumnusuru aliyedhulumiwa, na kuitika wito wa mwenye kualika (au kuita), na kutoa salamu, na akatukataza kuvaa pete za dhahabu, na kunywa katika vyombo vya madini ya fedha, na kukalia matandiko ya hariri, na kuvaa kassi (nguo iliyotengenezwa kwa katani na hariri) na kuvaa hariri nyepesi na hariri nzito na dibaji.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الترجمة

ar bs en es fa fr id ru tr ur zh hi ha pt ml ku vi nl as gu si hu ka ro

الشرح

Aliwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake waislamu mambo saba na akawakataza mambo saba; yale aliyowaamrisha ni: La kwanza: Kumtembelea mgonjwa. La pili: Kusindikiza jeneza na kushiriki katika kumswalia na kumzika, na kumuombea dua. La tatu: Kumuombea dua aliyepiga chafya na akamhimidi Mwenyezi Mungu, kwa kumuambia: Yar-hamukallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu). La nne: Kumuepusha aliyetoa kiapo na kumuamini, yaani ikiwa litaapiwa jambo hali yakuwa unauwezo wa kumuepusha na tuhuma basi fanya hivyo; ili usimpelekee kulipa kafara kwa kiapo chake. La tano: Kumsaidia aliyedhulumiwa, kwa kumtetea na kuyazuia yanayotokea kwake miongoni mwa dhulma, kwa kadiri ya uwezo. La sita: Kumuitikia mwenye kualika katika walima wa chakula, kama walima wa harusi, au akika, au kinginecho. La saba: Kutangaza utoaji wa salamu na kuuneza na kujibu pia. Na aliyoyakataza ni: La kwanza: Kuvaa pete za dhahabu na kujipamba nazo. La pili: Kunywa kwa kutumia vyombo vya fedha. La tatu: Kukaa katika matandiko, nayo ni magodoro ambayo huwekwa juu ya mgongo wa farasi, na juu ya ngamia, yaliyotengenezwa kwa hariri. La nne: Kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa katani ikachanganywa na hariri, na huitwa (Qassi). La tano: Kuvaa hariri. La sita: Kuvaa hariri nzito. La saba: Kuvaa dibaji, nayo ni: Aina bora zaidi ya hariri na ghali zaidi.

فوائد الحديث

Kumebainisha sehemu katika haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu.

Asili ni kuwa kila amri zinazokuja katika sheria au makatazo zinawahusu wanaume na wanawake, isipokuwa yaliyofanywa kuwa maalumu kwa wanaume au wanawake.

Hadithi nyingine zimeonyesha juu ya kumkataza mwanamke kusindikiza jeneza.

Zimeonyesha hadithi nyingine kufaa kuvaa dhahabu na hariri kwa mwanamke.

التصنيفات

Adabu za kisheria., Kumbeba maiti na kumzika.