Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala?

Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala?

Kutoka kwa Muadha amesema: Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala? Akasema: Hivi wewe ni mtu kutoka Haruuraa? (mji walikozusha fitina baina ya waislamu) Akasema: Hapana: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hilo, tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishwi kulipa swala.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Muadhi alimuuliza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Kwa nini mwenye hedhi analipa swaumu na wala halipi swala?. Akasema kumwambia: Hivi wewe ni katika Makhawariji (wanaotoka katika utiifu wa kiongozi wao) wa mji wa Haruuraa wanaokithirisha maswali kwa kutaka ugumu na kutia mkazo katika dini? Akasema: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hedhi tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishiwi kulipa swala.

فوائد الحديث

Kumkemea kila mwenye kuuliza swali la ukorofi na mjadala usio na faida.

Haruuria imenasibishwa na mji ulioko karibu na Kufa (Iraq), na unaitwa "Haruuraa": kulikuwa na kundi la Makhawariji (wanaojitoa katika kumtii kiongozi wao), alimfananisha nao katika mambo yao, na wingi wa maswali yao, na ukaidi wao.

Mwalimu anatakiwa kumbaini aliyemtaka kujifunza na kumpa muongozo.

Kujibu kwa nukuu ni bora; kwa sababu Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ziwe juu yake, hakujali maana aliyoikusudia muulizaji; na hii ni kwa sababu kujibu kwa hoja hukata zaidi mzozo.

Kujisalimisha katika hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, hata kama mja hatojua hekima yake.

Amesema Nawawi: Maana ya kauli ya Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa kundi katika Makhawariji (wanaotoka katika kuwatii viongozi) humuwajibishia mwenye hedhi kulipa swala zilizompita wakati wa hedhi, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya waislamu, na kiulizo hiki alichotumia Aisha kumuuliza ni kiulizo cha kumkemea mtu, yaani: Huu ni mfumo wa Haruria na ni mfumo mbaya mno.

التصنيفات

Hedhi Nifasi na Damu ya Ugonjwa., Kuilipa funga.