Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia

Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia

Kutoka kwa Anas bin Malik- Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Allah- Rehma na amani ziwe juu yake- "Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]

الشرح

Haepukani mwanadamu na kukosea, kwa jinsi alivyoumbwa kutokana na udhaifu, na kutokumtii msimamizi wake katika kutekeleza yale aliyomtaka ayafanye, na kuacha yale aliyomkataza, lakini yeye Mtukufu amefungua mlango wa toba kwa waja wake, na akaeleza kuwa mbora wa wakosefu ni wale wenye kukithirisha toba.

فوائد الحديث

Katika mambo ya mwanadamu ni kukosea na kuingia katika dhambi. La msingi kwa muumini atakapojiiingiza katika maasi afanye haraka kuleta toba.

التصنيفات

Toba