إعدادات العرض
Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu
Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu
Kutoka kwa Ikrima: Ya kwamba Ally radhi za Allah ziwe juu yake aliwachoma watu fulani, zikamfikia taarifa Bin Abbas akasema: Lau ningelikuwa mimi nisingewachoma, kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu", na ningewaua tu kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayebadili dini yake basi muuweni".
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Русский हिन्दी 中文 Bahasa Indonesia اردو Kurdî Português دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული বাংলা ไทย অসমীয়া Hausa Nederlands ਪੰਜਾਬੀ Tagalogالشرح
Alijitahidi Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akawachoma watu fulani kwa moto, miongoni mwa mazandiki walioritadi kutoka katika Uislamu, zikamfikia taarifa Abdallah bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, akamuunga mkono kwa kuwauwa kwake; lakini akakemea kuwachoma kwa moto. Na akasema: Lau ningelikuwa katika nafasi yake nisingeliwachoma kwa moto; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake alibainisha kuwa haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa moto, lakini inatosha tu kuwauwa, kwani alisema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu na akabadili dini yake kwa dini nyingine basi muuweni.فوائد الحديث
Uwajibu wa kumuuwa aliyeritadi kutoka katika dini yake kwa makubaliano ya wanachuoni, nayo inakuwa kwa sharti zake, na haruhusiwi yeyote kufanya hivyo isipokuwa kiongozi na hakimu.
Kauli yake: "Atakayebadili dini yake, basi muuweni" Yaani: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu: Hii ni huku ya watu wote kwa wanaume na wanawake.
Aliyeritadi haachwi katika kuritadi kwake bali ataitwa katika Uislamu, asipokubali ndio atauliwa.
Katika hadithi hii kuna katazo la kuadhibu kwa moto, na kwamba mipaka ya sheria haitekelezwi kwa moto.
Ubora wa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao, na upana wa elimu yake na utambuzi wake wa hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Hapa kuna adabu ya kumkemea aliyekosea.
التصنيفات
Adhabu ya mwenye kuritadi.