Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)

Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)

Kutoka kwa Abuu Umama Al-Bahiliy radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akasema: Wasemaje kuhusu mtu aliyepigana vita akitaka malipo kwa Allah na kusemwa vizuri na watu, ana lipi? Akasema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Akalirudia hilo mara tatu, akimwambia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Kisha akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)".

[Sahihi] [Imepokelewa na An-Nasaaiy]

الشرح

Alikuja mtu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kumuuliza na kumuuliza juu ya hukumu ya mtu anayetoka kwa ajili ya vita na jihadi kutafuta malipo kwa Mwenyezi Mungu na kutaka sifa na pongezi kwa watu, je anapokea thawabu? Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akajibu: Huyo hana malipo yoyote. Alipochanganya kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu katika nia yake, yule bwana akarudia swali lake mara tatu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na akamjibu na akathibitisha jibu lile lile kwake kwamba hana malipo, basi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, akampa kanuni ya kukubalika amali kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Mwenyezi Mungu haikubali amali isipokuwa yote iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bila ya yeyote kuhusishwa nayo, na iwe ni kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile iliyotakaswa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kulingana na muongozo wa Mtume wake -rehema na amani ziwe juu yake.

Ni kuwa katika uzuri wa majibu ya mtoaji wa Fat'wa yatosheleze swali la muulizaji na zaidi.

Kulitia mkazo jambo kubwa kwa kurudia swali.

Mpiganaji wa kweli ni yule atakayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, na kwa kutafuta malipo na thawabu za Akhera pamoja na kutakasa nia, ili kupigana kwake kusiwe ni kwa ajili ya dunia.

التصنيفات

Fadhila za matendo ya moyoni.