Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi

Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi

Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa peponi kuna daraja na vituo mia moja, na masafa yaliyopo kati ya daraja mbili ni kama masafa kati ya mbingu na ardhi, na Pepo ya juu zaidi miogongoni mwa Pepo hizi ni Pepo ya Firdausi, na ndani yake ndiko inapochimbuka mito yote minne ya Pepo, na juu ya Firdausi ndiko inakokuwa Arshi; mkimuomba Mwenyezi Mungu basi muombeni Firdausi; kwani ndiyo iko juu ya Pepo zote.

فوائد الحديث

Kutofautiana kwa vituo vya watu wa Peponi, na hii ni kulingana na imani na mtendo mema.

Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu Firdausi ya juu katika Pepo.

Firdausi ndiyo Pepo ya juu, na ndio bora zaidi kuliko zote.

Ni wajibu kwa muislamu hamu yake kuwa ya juu zaidi, na aende mbio na aombe makazi ya juu na bora zaidi kuliko yote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mito minne ya Pepo ni mito ya maji na maziwa na mvinyo na asali iliyotajwa ndani ya Qur'ani katika kauli yake Mtukufu: "Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wachamungu, ndani yake kuna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa" [Muhammadi: 15].

التصنيفات

Kuamini siku ya mwisho, Maisha ya Akhera., Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.