Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake

Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake

Kutoka kwa Abul Ja'di Adh-dhwamri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa na uswahaba, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"

[Sahihi]

الشرح

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.

فوائد الحديث

Ameeleza bin Mundhiri kuwa kuna makubaliano ya wanachuoni wote kuwa swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila mtu.

Ahadi mbaya kwa atakayeacha swala ya Ijumaa kwa kupuuza, kwamba Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake.

Atakayeacha swala ya Ijumaa kwa dharura huyu haingii katika ahadi hii mbaya.

Amesema Shaukani: Kauli yake: (Ijumaa tatu), inategemea maana mbili, kuacha kwa ujumla sawa sawa zimefuatana Ijumaa hizo au zimetofautiana, hata akiacha katika kila mwaka Ijumaa moja basi Mwenyezi Mungu angepiga muhuri juu ya moyo wake baada ya Ijumaa ya tatu, na ndivyo hadithi inavyoonyesha, na maana ya pili nikuwa inakusudiwa Ijumaa tatu mfululizo.