إعدادات العرض
Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini
Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.
الترجمة
العربية Tiếng Việt Bahasa Indonesia Nederlands English অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Aliweka kikomo Mtume rehema na amani ziwe juu yake cha mtu kupunguza sharubu, na kupunguza kucha za mikono na miguu, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, kusizidi kuziacha kwake zaidi ya siku arobaini.فوائد الحديث
Amesema Shaukani: Kilicho sawa nikuwa adhibiti kwa arobaini aliyoidhibiti kwayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake haitakiwi kuivuka, na haitochukuliwa kama kwenda kinyume na sunna kwa kuacha kupunguza na mfano wake baada kurefuka mpaka ifike kikomo cha muda huo.
Amesema bin Hubaira: Hadithi hii ndio kikomo cha kuchelewesha hilo, na kilichobora ni kulitekeleza hilo kabla ya ukomo huo.
Uislamu umetilia kipaumbele usafi na kujitwaharisha na kujipamba.
Kupunguza sharubu, kwa kunyoa nywele zinazoota juu ya mdomo wa juu.
Kukwapua nywele za kwapa, kwa kuondoa nywele zinazoota humo, nayo ni sehemu inayokuwa chini ya maungio kati ya mkono na bega.
Kunyoa nywele za siri, nazo ni nywele zinazoota pembezoni mwa tupu ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke.
التصنيفات
Sunna za Kimaumbile.