Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya

Kutoka kwa Ally bin Abii Twalib, na Mua'dh bin Jabali- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya imamu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, ima ya kusimama au kurukuu au kusujudu au kukaa, basi aendane na imamu pale alipo katika kusimama au kurukuu au kitendo kinginecho, na asisubiri mpaka anyanyuke imamu kama wanavyofanya baadhi ya watu.

فوائد الحديث

Sheria ya kuingia mwenye kuungana pamoja na imamu katika kipengele chochote miongoni mwa vipengele vya swala atakachokikuta, bila kutofautisha kati ya rukuu na sijida na kukaa.

Nikuwa kuipata rakaa ambayo ameungana na imamu kunakuwa kwa kuikuta rukuu yake, kama zilivyoonyesha juu ya hilo dalili zingine.

التصنيفات

Hukumu ya Imamu na Maamuma.