Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao

Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliingia Hindu binti Utba mke wa Abuu Sufiani kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Abuu Sufiani ni mwanaume bahili sana, hanipi matumizi yanayonitosha mimi na wanangu isipokuwa kiasi ninachokichukua katika mali yake pasina yeye kujua, je kwa hilo nina tatizo? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kutoa mahitaji kwa mke na watoto.

Amesema bin Hajari: Na makusudio ya kauli yake: "Chukua katika mali yake kiasi kinachokutosha kwa wema", akamuelekeza katika wema kwa kiasi ambacho hakina kiwango katika sheria.

Amesema bin Hajari: Hadithi hii imetumika kama ushahidi wa kuruhusu kumtaja mtu kwa yale asiyoyapenda ikiwa katika mfumo wa kuuliza na kulalamika na mfano wake, na hii ni moja kati ya sehemu ambazo hi halali ndani yake kusengenya.

Amesema Qurtubi: Hindu hakukusudia kumsifia Abuu Sufiani kwa ubahili kwa hali zote, bali alieleza hali yake akiwa naye na kwamba yeye alikuwa akimtiadhiki yeye na wanaye, na hii haimaanishi ubahili wa moja kwa moja, kwani viongozi wengi hufanya hivyo kwa familia zao na huwaathiri sana upande wa kujenga mapenzi nao.

التصنيفات

Matumizi.