إعدادات العرض
Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo
Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo
Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português മലയാളം Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlandsالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.فوائد الحديث
Fadhila za kuvumilia balaa, na kuacha kuchukia na kulalamikia maumivu, ili hilo lisipelekee katika jambo baya zaidi kuliko hilo.
Kuhadithia kuhusu Umma zilizopita kwa yale ambayo yana kheri na mawaidha ndani yake.
Amesema bin Hajari: Hapa kuna kusimama katika haki za Mwenyezi Mungu na rehema zake na kwa viumbe wake, kiasi ambacho amewaharamishia kujiua, na kwamba nafsi ni milki ya Mwenyezi Mungu.
Uharamu wa kutumia sababu zinazopelekea katika kuia nafsi, na onyo kali katika hilo.
Amesema bin Hajari: Na imeonyesha kuwa alijikata kwa ajili ya kujiua na si kwa kutaka kujitibu, ambayo inaweza kuwa dhana ya kunufaika na kitendo hicho.
التصنيفات
Kuyasema vibaya Maasi.