إعدادات العرض
Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho
Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hatuweki mikono yetu mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi anaweka mkono wake, na hakika sisi kuna wakati tulihudhuria chakula pamoja naye, akaja kijakazi kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akamshika mkono wake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho, na bila shaka alikuja na kijakazi huyu ili akihalalishe, nikashika mkono wake, akaja tena na Bedui huyu ili akihalalishe nikamshika mkono, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wake umekamatwa na mkononi wangu pamoja na mkono wake kijakazi".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Română অসমীয়াالشرح
Ameeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.فوائد الحديث
Heshima ya Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na adabu yao kwake.
Katika adabu za chakula ni mdogo kusubiri mpaka aanze mkubwa na mwenye heshima katika kula.
Shetani huwasukuma baadhi ya watu wanaojisahau katika matendo ambayo yeye anayapenda; ili aweze kufikia lengo lake, na miongoni mwake ni haya yaliyoko katika hadithi hii.
Anasema Nawawi: Wanasema Wanachuoni: Na inapendeza mtu kutamka kwa sauti Bismillaah ili mwenzake asikie na amzindue kwa hilo.
Nikuwa atakapokuja mtu anataka kula na ukawa hujamsikia anasema Bismillaah basi mshike mkono wake mpaka aseme Bismillaah.
Uwajibu wa kuondoa uovu kwa mwenye kujua, na kuondoa uovu kwa mkono kwa mwenye uwezo.
Hadithi hii ni alama niongoni mwa alama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjulisha kilichotokea katika kisa hiki.
Shetani hapati uwezo wa kula chakula cha watu wenye imani isipokuwa kama wasipotaja jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho.
Inapendeza kuwafundisha watu adabu za kula na kunywa katika Uislamu.
Inapendeza kutoa kiapo; kwa ajili ya kusisitiza jambo kwa msikilizaji.
Amesema Nawawi: Bismillaah wakati wa kunywa maji na maziwa na Asali na mchuzi na dawa na vinywaji vinginevyo ni kama Bismillaah wakati wa chakula.
Amesema Nawawi: Na ikiwa mtu ataacha Bismillaah mwanzo wa chakula kwa makusudi au kwa kusahau au kwa ujinga au kwa kulazimishwa au kwa kushindwa kwa sababu yoyote ile iliyojitokeza, kisha akaweza kufanya hivyo wakati wa kula kwake, basi ni sunna aseme: "Bismillaahi Awwalihi wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Akatapokula mmoja wenu basi na ataje jina la Mwenyezi Mungu, na ikiwa atasahau kumtaja Mwenyezi Mungu mwanzo wa chakula, basi na aseme: Bismillaahi Awwalihi Wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake". Kaipokea Abuu Daudi na Tirmidhi.
التصنيفات
Adabu ya kula na kunywa.