إعدادات العرض
1- Hakika Mwenyezi Mungu huridhika kwa mja anapokula chochote, akamshukuru juu ya hicho, au akanywa chochote akamshukuru juu ya hicho.
2- Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na ule kwa mkono wako wa kulia, na ule chakula kilicho mbele yako" kinachokuelekea"
3- Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani shetani anakula kwa mkono wako wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto
4- Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea.
5- Yakwamba mtu mmoja alikula kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa mkono wake wa kushoto, akasema: kula kwa mkono wako wa kulia, akasema: siwezi. akasema: Hutoweza, hakuna kilichomzuia isipokuwa ni kiburi, basi hakuweza tena kuunyanyua kufika kinywani kwake