Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho

Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa shukurani za mja kwa Mola wake Mlezi juu ya fadhila zake na neema zake ni miongoni mwa mambo ambayo huleta radhi za Allah; akala chakula akasema: Al-hamdulillah, na akanywa kinywaji na akasema: Al-hamdulillah.

فوائد الحديث

Ukarimu wa Allah Mtukufu, ametoa fadhila zake kwa riziki na kisha akaridhia shukurani.

Radhi za Allah hupatikana kwa sababu nyepesi, kama kushukuru baada ya kula na kunywa.

Katika adabu za chakula na kinywaji: Ni kumshukuru Allah Mtukufu baada ya kula na kunywa.

التصنيفات

Adabu ya kula na kunywa.