Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto

Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anamuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu ale na anywe kwa mkono wake wa kulia, na anakataza kula na kunywa kwa mkono wa kushoto; na hii ni kwa sababu Shetani anakula na anakunywa kwa kushoto.

فوائد الحديث

Katazo la kujifananisha na Shetani kwa kula au kunywa kwa kushoto.

التصنيفات

Adabu ya kula na kunywa.