إعدادات العرض
Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji
Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Tiếng Việt Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango mmoja miongoni mwa milango ya Pepo unaitwa: Mlango wa Rayyan, wataingia hapo wafungaji siku ya Kiyama, hatoingia yeyote zaidi yao, patanadiwa: Wako wapi wafungaji, basi watasimama na wataingia, hatoingia hapo yeyote zaidi yao, atakapomaliza kuingia wa mwisho wao utafungwa, na hatoingia tena yeyote.فوائد الحديث
Amesema Nawawi: Katika hadithi hii kuna ubora wa swaumu na heshima kwa wafungaji.
Mwenyezi Mungu amewatengea wafungaji mlango katika milango minane ya Pepo, watakapouingia utafungwa.
Kumebainishwa kuwa Pepo inamilango.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Wako wapi wafungaji", yaani: Wenye kukithirisha kufunga, kama mtu muadilifu na dhalimu, husemwa kwa mtu aliyezoea hilo, na si kwa mwenye kufanya hilo mara moja.
"Rayyan" Yaani: Mwenye kukata kiu; kwa sababu wafungaji hupata kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi zenye joto la muda mrefu; watalipwa kwa kuitwa mlango huu kwa kile kilichokuwa kinawahusu wao, mlango wa Rayyan, na imesemekana kuwa Rayyan ni wingi wa kulowesha koo kinyume cha kiu, na umeitwa hivyo; kwa sababu ndio malipo ya wafungaji kwa kiu yao na njaa yao.
التصنيفات
Ubora na Fadhila za Funga.