إعدادات العرض
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Nederlands Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو ไทย മലയാളം नेपालीالشرح
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipitiliza katika kufanya aina mbalimbali za kheri na aina za wema na ibada zaidi kuliko namna anavyojitahidi katika siku zingine; na hii ni kwa sababu ya utukufu na fadhila za siku hizi, na ni kwa sababu ya kuitafuta Lailatul Qadri (usiku wa cheo).فوائد الحديث
Himizo la kukithirisha kutenda wema na aina mbalimbali za ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ujumla na hasa hasa siku kumi za mwisho.
Siku kumi za mwisho wa Ramadhani zinaanzia usiku wa tarehe ishirini na moja mpaka mwisho wa mwezi.
Ni sunna kufaidika na nyakati bora kwa ibada.