Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake

Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake

Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Huraira, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, alisema siku ya (vita vya) Khaibar: "Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake". Akasema Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sikuwa napenda uongozi wakati huo, fikra zikanipelekea kuwa na matarajio ya kuitwa kwa ajili ya bendera hiyo, akamuita Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Ally bin Abii Twalib -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akampa bendera hiyo, na akasema: "Nenda na usigeuke mpaka Mwenyezi Mungu akufungulie" Akatembea Ally mwendo kidogo kisha akasimama na wala hakugeuka kisha akazungumza kwa sauti ya juu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa lipi niwapige watu? Akasema: "Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakifanya hivyo watakuwa wamekinga kwako damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki yake, na hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Aliwaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kuhusu ushindi wa waislamu kesho dhidi ya Mayahudi wa mji wa Khaibar ambao ni mji uko karibu na Madina, na hii ni kupitia mkono wa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera inayofanywa na jeshi kama nembo, na mtu huyu miongoni mwa sifa zake nikuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda pia. Na alieleza Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake kuwa hapendi uongozi na hapendi kuwa yeye ndiye anayelengwa isipokuwa kwa siku hiyo; kwa kutaraji yampate aliyoyasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Omari akanyanyua mwili wake ili auone Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kutaraji kuwa anaweza kuitwa kwa ajili ya hilo, na akiwa na pupa na tamaa ya kuchukua bendera hiyo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akampa bendera, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha jeshi litembee, na lisiondoke katika vita baada ya kukutana na maadui sawa iwe ni kwa mapumziko au kwa kusitisha au kutuliza vita, mpaka Mwenyezi Mungu amfungulie ngome hizi kwa ufunguzi na ushindi. Akatembea Ally radhi za Allah ziwe juu yake, kisha akasimama isipokuwa hakugeuka; ili asiende kinyume na amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi Ally radhi za Allah ziwe juu yake akanyanyua sauti yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nipigane na watu kwa lipi?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ikiwa watalikubali hilo, na wakaingia ndani ya Uislamu; watakuwa wamezizuia kwako damu zao na mali zao, na zitakuwa haramu kwako, isipokuwa kwa haki yake, yaani: Isipokuwa kama watafanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kuuawa kwa kosa hilo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, na hesabu yao itakuwa kwa Mwenyezi Mungu.

فوائد الحديث

Maswahaba walikuwa wakichukia uongozi kwa sababu ndani yake kuna majukumu makubwa.

Inafaa kuchunguza na kufuatilia kwa ajili ya kuhakiki uzuri wa jambo.

Kiongozi mkuu anatakiwa kumpa maelekezo kamanda wa jeshi katika namna ya kuchukua maamuzi katika kiwanja cha mapambano.

Maswahaba wa Mtume kushikamana na usia wake na kwenda mbio kuutekeleza.

Anayetatizwa na jambo katika yale aliyoelekezwa basi anauliza.

Miongoni mwa dalili za unabii wake rehema na amani ziwe juu yake ni kutoa kwake habari ya ushindi juu ya Mayahudi, kiasi ambacho alieleza kuhusu kuufungua mji wa Khaibar na ikatokea kama alivyoeleza.

Himizo la kuyaendea haraka yale aliyoyaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Hairuhusiwi kumuua aliyetamka shahada mbili isipokuwa yakionekana kwake yanayopelekea kuuawa.

Hukumu za Uislamu zinakwenda katika yale yanayodhihiri kwa watu, na Mwenyezi Mungu ndiye anayesimamia siri zao.

Lengo kubwa la Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu.

التصنيفات

Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.