Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu

Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu

Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".

[Sahihi]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume muislamu katika kikoi chake, nacho ni kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume, kwa hali tatu: Ya kwanza: Inayopendeza iwe kati kati ya muundi. Ya pili: Inayojuzu pasina karaha ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili; nayo ni mifupa miwili iliyotokeza katika maungio ya muundi na mguu. Ya tatu: Iliyoharamishwa, nayo ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili, na inahofiwa kwake kupatwa na adhabu ya moto, na ikiwa ni kwa kiburi na kwa kufurahia na ujeuri, Mwenyezi Mungu hatomtazama.

فوائد الحديث

Sifa hii na ahadi hii ya adhabu ni maalumu kwa wanaume, ama wanawake, wanaondolewa katika hilo; kwa sababu wao wameamrishwa kusitiri mwili wao wote.

Kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume huitwa kikoi; kama suruali, na nguo na vinginevyo, na vyote hivyo vinaingia katika hukumu ya kisheria iliyotajwa katika hadithi.

التصنيفات

Adabu za kuvaa.