Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy]

الشرح

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.

فوائد الحديث

Ubora wa dua hii na kujibiwa kwake.

Muumini anapupia kuepuka tabia mbaya na matendo maovu, na anachukua tahadhari ya kufuata matamanio na kutumbukia katika matamanio.

Kugawanyika kwa tabia na matendo na matamanio katika maovu na mazuri.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.