إعدادات العرض
Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo
Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlandsالشرح
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.فوائد الحديث
Kutosheka ni miongoni mwa tabia tukufu za muumini, nayo ni katika alama za kuridhia makadirio ya Mwenyezi Mungu.
Amesema bin Jariri: Hii ni hadithi iliyokusanya aina nyingi za kheri; kwa sababu mtu anapoona mtu aliyefadhilishwa katika dunia basi hutamani apate mfano wake, na kuyadogesha aliyonayo katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anapata tamaa ya kuongeza ili amfikie huyo au amkaribie, hili ndilo liliopo kwa watu wengi, na ama akimtazama katika mambo ya kidunia yule aliye chini yake katika yale yaliyodhihiri kwake katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu anazomzidi, akamshukuru na akanyenyekea, na akafanya kheri ndani yake.
التصنيفات
Kuzitakasa Nafsi.