Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi

Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi

Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuburuza nguo au kikoi chini ya kongo mbili kwa kiburi na kujiona, nakuwa mwenye kufanya hivyo atastahiki ahadi ya adhabu kali yakuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya Kiyama mtazamo wa huruma.

فوائد الحديث

Nguo inakusanya kila kinachositiri chini ya mwili, kuanzia suruali na nguo na kikoi na vinginevyo.

Katazo la kupitiliza nguo mpaka chini ni maalumu kwa wanaume pekee, amesema Nawawi: Na wamekubaliana wanachuoni juu ya kufaa kuburuza nguo kwa wanawake, na imesihi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapa idhini ya kuburuza nguo zao kwa kiasi cha dhiraa moja.

Amesema bin Bazi: Kupitiliza nguo kumekatazwa na ni haramu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi, na ama adhabu, zinatofautiana, na wala si lazima zote ziwe sawa, kwa sababu aliyekusudia kujifaharisha hawezi kuwa sawa na ambaye hajakusudia.

Amesema bin Bazi: Mwanamke ni uchi hakuna tatizo kwake kushusha nguo kwa kiasi cha nchi tano, ikiwa haitamtosha basi atashusha kiasi cha dhiraa (futi) kuanzia katika kongo mbili.

Amesema Kadhi: Wamesema wanachuoni: Na kwa ujumla inachukiza kila kilichozidi juu ya haja na mazoea katika nguo, katika urefu na upana, na Allah ndiye Mjuzi zaidi.

Amesema Nawawi: Kiasi kinachopendeza katika sehemu inayoshuka katika kanzu na kikoi ni nusu ya miundi, na hakuna ubaya kama kitakuwa kati yake na kongo mbili, na kitakachoshuka zaidi ya hapo ni sababu ya kuingia motoni, inayopendeza ni nusu ya miundi, na inayofaa pasina karaha ni chini yake mpaka katika kongo mbili, kitakachoshuka chini ya kongo mbili hicho kimekatazwa.

Amesema bin Uthaimiin katika kauli yake: "Mwenyezi Mungu hatomtazama" Yaani mtazamo wa huruma na upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka hakifichikani kwake kitu chochote, na wala hakitoweki machoni mwake chochote, lakini makusudio yake ni mtazamo wa huruma na upole.

التصنيفات

Adabu za kuvaa.