Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa

Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud]

الشرح

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapofikiwa na asubuhi nayo ni mwanzo wa mchana pamoja na kuchomoza Alfajiri anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka" tukiwa tumegubikwa na hifadhi yako na kufunikwa na neema zako, tukishughulika na kukutaja, tukitaka msaada kwa jina lako, tukienewa na taufiki yako, tukifanya harakati zenu kwa ujanja wako na nguvu zako, "na kwako tumeshinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa" yaani; hii ni kama lafudhi iliyotangulia isipokuwa hii imefanywa ya jioni, atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwa jina lako Muhuishaji tunakuwa hai, na kwa jina lako Mfishaji tutakufa, "na kwako tutafufuliwa" na kufufuliwa baada ya kifo, na kusambaa baada ya kukusanywa, itaendelea hali yetu namna hii katika nyakati zote, na hali zingine zilizobakia, na wala sitoachana nayo wala sitoihama. Na ikimfikia jioni baada ya Lasiri atasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutafuka, na marejeo ni kwako" na marejeo katika dunia, na mafikio katika mwisho, wewe ndiye unayenihuisha na wewe ndiye unayenifisha.

فوائد الحديث

Inapendeza kusoma dua hii asubuhi na jioni, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Uhitaji wa mja kwa Mola wake Mlezi katika hali zake na nyakati zake zote.

Kilicho bora katika kusoma Adhkari, asubuhi ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na baada ya Laasiri mpaka kabla ya kuzama, ikiwa atazisoma baada ya hapo, yaani: Asubuhi akazisoma baada ya Jua kunyanyuka itafaa, na hata akizisoma baada ya Adhuhuri itafaa pia, na akizisoma baada ya Magharibi itafaa, huo ndio wakati wa kufanya Adhkari.

Mahusiano kati ya kauli yake "na kwako tutafufuliwa" na kusemwa asubuhi, kauli hii inamkumbusha kuhuishwa na kufufuliwa kukubwa pindi watapokufa watu na kufufuliwa siku ya Kiyama, huku ni kufufuliwa kupya, na siku mpya ambayo hurejeshwa roho ndani yake, na watu hutawanyika ndani yake, na wanapumua katika asubuhi hii mpya aliyoiumba Mwenyezi Mungu; ili iwe shahidi kwa mwanadam, na ili ziwe nyakati zake mida yake ni hazina ya matendo yetu.

Mahusiano kati ya kauli yake "Na kwako ndio mafikio" na kusemwa jioni, ni pale watakaporejea watu katika matendo yao na kutawanyika kwa kwenda katika masilahi yao na maisha yao, wanarejea katika nyumba zao, na wanadumishwa katika raha baada yakuwa wametawanyika, inamkumbusha kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa hatima na marejeo na mafikio.

التصنيفات

Nyiradi za Asubuhi na Jioni.