إعدادات العرض
Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu
Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu
Kutoka kwa Abuu Umama Al-Baahili radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Walitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu wawili, mmoja wao mchamungu na mwingine msomi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu", Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake na wakazi wa mbinguni na ardhini hata mdudu chungu katika shimo lake na hata samaki humtakia rehema mwenye kuwafundisha watu mambo ya kheri".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Română অসমীয়াالشرح
Walitajwa watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mmoja wao ni mchamungu, na mwingine msomi, ni yupo mbora kati yao? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ubora wa msomi wa elimu ya kisheria mwenye kuifanyia kazi na mwenye kuifundisha kwa mchamungu aliyejitenga kwa ajili ya ibada, pamoja na kujua kwake yale ya wajibu kwake katika elimu ni kama ubora wake rehema na amani ziwe juu yake na utukufu wake kwa Swahaba wa chini zaidi. Kisha akabainisha rehema na amani ziwe juu yake sababu ya hilo, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake miongoni mwa wabeba Arshi, na wakazi wa mbinguni katika Malaika wengineo, na wakazi wa Ardhi kwanzia binadam na majini na wanyama wote, hata mdudu chungu katika makazi yake ndani ya tumbo la Ardhi, na hata nyangumi na samaki wa Baharini; alitaja hivi ili waingie katika kauli hii viumbe wa nchi kavu na Baharini, wote hawa wanamuombea mazuri mwenye kuwafundisha watu elimu ya dini ambayo ndani yake kuna uokovu wa watu na mafanikio yao.فوائد الحديث
Miongoni mwa nyenzo za kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni kuhamasisha na kupiga mifano.
Ukubwa wa utukufu wa wanachuoni, wale waliojifunza elimu na wakatekeleza haki yake, kama kuifanyia kazi na kuifikisha.
Himizo la kuwaheshimu wanachuoni na wanafunzi, na kuwaombea dua.
Himizo la kwafundisha watu mambo ya kheri; kwa sababu ndio kufaulu kwao na furaha yao.
التصنيفات
Ubora wa Elimu.