إعدادات العرض
Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama
Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama" Yaani: Upepo yake.
الترجمة
العربية Bosanski English فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी Español Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Românăالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayejifunza elimu ya kisheria ambayo asili yake ni kutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa apate heshima na starehe za kidunia miongoni mwa mali au cheo, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama.فوائد الحديث
Uwajibu wa kutakasa nia katika kutafuta elimu, na himizo juu ya hilo.
Tahadhari kubwa ya kuichukua elimu ya kisheria kwa kujionyesha au daraja la kuifikia dunia, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
Nikuwa atakayeitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ikamuijia dunia yenyewe inafaa kwake kuichukua, na hilo halitomdhuru.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Harufu ya Pepo" Neno harufu limetumika likiashiria kupita kiasi katika kuharamishwa Pepo; kwa sababu asiyeweza kupata harufu ya kitu hawezi kukipata.
Atakayejifunza elimu katika yale ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu kwayo, kwa ajili ya kupata ajira, au kwa ajili ya malengo mengine; basi anatakiwa kutubia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo, na Mwenyezi Mungu atamfutia yaliyojitokeza miongoni mwa nia mbaya, kwani Yeye anafadhila kubwa Aliyetakasika na kutukuka.
Tahadhari hii ni kwa mwenye kutafuta elimu ya kisheria, ama atakayetafuta elimu yoyote katika elimu za kidunia kwa ajili ya starehe za dunia, kama uhandisi, na kemia, na mengineyo kwa ajili ya masilahi ya dunia, hakuna shaka atalipwa kwa nia yake.