Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf

Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf

Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."

فوائد الحديث

Kumebainishwa fadhila ya suratul Kahaf, na kuwa mwanzo wake na mwisho wake zinakinga na fitina za Dajali.

Kumeelezwa swala la Dajali, na kumebainishwa yanayokinga na fitina hiyo.

Himizo la kuihifadhi suratul Kahaf nzima, ikiwa atashindwa basi ahifadhi aya kumi za mwanzo na za mwisho.

Amesema Al-Qurtubi katika sababu ya hilo: Imesemekana: Kwa sababu ya yale yaliyoko ndani ya kisa cha watu wa pangoni katika maajabu na miujiza, atakayeizingatia hatoshangazwa na jambo la Dajali na halitamtisha hilo na wala hatofitinika, na imesemekana: Kwa sababu ya kauli yake Mtukufu: "Ili kitoe onyo kali kutoka kwake" Kwa kuuhusisha ugumu na ukali na kwake, na ndio unafaa kwa yale atakayokuwa nayo Dajali katika kudai uungu na kutawala kwake na ukubwa wa fitina yake, inakuwa maana ya hadithi nikuwa: atakayesoma aya hizi na akazizingatia na akasimama katika maana zake zitamtahadharisha na atasalimika naye.

التصنيفات

Fadhila za Sura na Aya., Alama za Kiama .